Simba yatajwa na CAF klabu tajiri zaidi Afrika
Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam imetajwa na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuwa klabu namba 5 kwa utajiri Barani Afrika.
Simba imetajwa kuwa na utajiri wa karibu Paund Milioni 10.35 ambayo ni sawa na Bilioni 32.3 kwa shilingi ya Tanzania.
Katika orodha hiyo Al Ahly kutoka Misri inaongoza ikiwa na utajiri wa Paund Milioni 19.25 ikifuatiwa na Esperance Sportive de Tunis (12.75M)na Club Africain (11.8M) zote kutoka Tunisia.
Ya nne ni Kaizer Chief ya kutoka nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inautajiri karibu Paund Milioni 10.48.
Klabu tajiri zaidi barani Afrika.
1. Al Ahly(Egypt) - €19,25M.
2. Esperance Sportive de Tunis( Tunisia)- €12,75M.
3. Club Africain ( Tunisia)- 11,80M
4. Kaizer Chiefs( South Africa)-€ 10,48M
5. Simba Sports Club (Tanzania)- €10,35M
6. Zamalek SC (Egypt) - €10,30M.
7. USM Alger( Algeria)- Market € 9,65M.
8. ES Serif ( Algeria)-8,60M.
9. Raja Casablanca( Morocco)- €8,13M
10. TP Mazembe( DRC)- €7,70M