AZAM FC KUIFUATA STAND UNITED NUSU FAINALI LEO?
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc usiku wa leo wanashuka katika uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi kuumana na Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Feferation Cup.
Jana Stand United imetangulia nusu fainali baada ya kuilaza Njombe Mji bao 1-0 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, kwa maana hiyo mshindi kati ya Azam Fc na Mtibwa Sugar atakutana na Stand United kwenye nusu fainali.
Mechi nyingine leo itapigwa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine pale Mbeya wakati wenyeji Tanzania Prisons wakiwaalika wanajeshi wa JKT Tanzania mchezo wa robo fainali wa michuano hiyo, kesho pia kutakuwa na mchezo mwingine Yanga Sc wakiwa wageni wa Singida United uwanja wa Namfua mjini Singida