Stand United yawa ya kwanza kutinga nusu fainali FA Cup

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga imefanikiwa kuwa timu ya kwanza kutangulia kuingia nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup, baada ya kuilaza Njombe Mji ya Njombe bao 1-0.

Mchezo huo wa robo fainali uliofanyika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 12 kipindi cha kwanza na Hamad Swahady aliyepokea pasi ya Vitalis Mayanga.

Hata hivyo Stand United walimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya nahodha wake Alex Mulilo kuonyeshwa kadi mbili za manjano, kesho michuano hiyo itaendelea kati ya Tanzania Prisons na JKT Tanzania huku usiku Azam Fc itaialika Mtibwa Sugar

Stand United imeingia nusu fainali

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA