KIUNGO YANGA ADAIWA KUTELEKEZA MTOTO, AFA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa klabu bingwa ya soka nchini, Yanga Sc, Geofrey Mwashiuya, inadaiwa ametelekeza mtoto na kwa bahati mbaya mtoto huyo amefariki dunia hivi karibuni baada ya kuungua na maji ya moto akiwa anacheza peke yake.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya majirani, zinasema kuwa mtoto huyo mdogo alikuwa akicheza peke yake kwa bahati mbaya akamwagikiwa na maji ya moto yaliyokuwa jikoni na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Mtoto huyo inadaiwa kuwa ni wa mchezaji huyo wa Yanga lakini taarifa zinasema kuwa Mwashiuya alishamkataa baada ya kuzaliwa na hakuwahi kumuona, ila mzazi mwenzake anathibitisha kuwa ni wa Mwashiuya kwani alikuwa rafiki yake wa muda mrefu.
Mtoa taarifa hizi anasema Mwashiuya alipigiwa simu kujulishwa kifo cha mwanaye lakini aliwajibu kuwa Yanga imemzuia kutoka kambini hivyo hawezi kuhudhuria mazishi.
Mungu ailaze mahari pema peponi roho ya mtoto huyo asiye na hatia yoyote