Yanga waiendea Moro, Singida United
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kikosi cha mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc leo kinatarajia kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa Robo fainali dhidi ya Singida United kombe la Azam Sports Federation Cup uwanja wa Namfua mjini Singida.
Yanga watasafiri na wachezaji wake wote isipokuwa wale waliopo kwenye timu za taifa za Taifa Stars na Ngorongoro Heroes.
Wachezaji ambao watakosekana kwenye msafara huo ni Ibrahim Ajibu, Hassan Kessy, Ramadhan Kabwili na Kevin Yondan, wengine ni Maka Edward na Said Musa "Ronaldo" ambao hao wapo na Ngorongoro Heroes.
Yanga ikishamaliza mchezo wake na Singida United, Aprili 1, itarejea Dar es Salaam kujiwinda na mchezo wa kuelekea hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia utakaopigwa Aprili 7 mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es Salaam