Taarifa za Mkude kuvunjika kifundo cha mguu hizi hapa

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kiungo mahiri na bora kwa sasa hapa nchini, Jonas Gerald Mkude jana amevunjika kifundo cha mguu akiwa katika mazoezi ya klabu yake ya Simba Sc  yaliyofanyika kwenye uwanja wa Boko Veteran.

Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka, zinasema kuwa kiungo huyo aliumia kifundo cha mguu na kushindwa kuendelea na mazoezi na kupelekea kurudishwa nyumbani kwake ni baada ya kufanyiwa rafu na kiungo mwenzake Muzamir Yassin.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe alishindwa kumpa matibabu kiungo huyo ili arejee mazoezi na badala yake alimruhusu aondoke huku akishindwa kukanyaga kwa miguu yote miwili kwani alikuwa akichechemea, Simba inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu bara dhidi ya Njombe Mji, Aprili 3 mwaka huu uwanja wa Sabasaba mjini Njombe hivyo kunatilia shaka uwepo wa Mkude katika mchezo huo.

Licha ya kuumia Mkude, jana majeruhi wawili wa muda mrefu, Haruna Niyonzima na Salim Mbonde wameanza mazoezi na kuna uwezekano mkubwa wa kuanza katika mchezo huo, Simba ndio kinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 46 lakini ikilingana na hasimu wake Yanga Sc

Jonas Mkude ameumia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA