Yanga yaikamata Simba kileleni
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kuilaza Stand United mabao 3-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Yanga walijipatia mabao mawili mapema, moja likifungwa dakika ya sita na Yusuphu Mhiru na lingine likifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 12, timu hizo zilienda kupumzika Yanga ikiwa mbele.
Kipindi cha pili Stand United walilishambulia lango la Yanga wakitaka kusawazisha na wakafanikiwa kupata bao kupitia Vitalis Mayanga, kabla ya Obrey Chirwa kufunga bao la tatu.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 46 sawa na mahasimu wao Simba Sc wanaoongoza ligi hiyo na sasa Yanga ni ya pili