ANAYEKUMBUKWA

ISSA ATHUMAN MGAYA: FUNDI WA MPIRA.

Alianza kujulikana kama fundi seremala akitengeneza vitanda, makochi na meza kwa kutumia mbao, ujuzi huo alifundishwa na mjomba wake ambaye alizaliwa tumbo moja na mama yake mzazi.

Hapa namzungumzia fundi wa mpira Issa Athuman Mgaya ambaye alicheza kwa mafanikio Yanga Sc na timu ya taifa, Taifa Stars miaka iliyopita.

Nakumbuka wakati huo nilikuwa mdogo lakini nilikuwa mfutiliaji mkubwa wa mpira wa miguu, Issa alikuwa kiungo mkabaji wa Yanga mwenye uwezo wa kucheza sentahafu na aliweza kung' ara vilivyo kwenye kikosi hicho na kubahatika kwenda kucheza soka la kulipwa Uarabuni.

Kwa miaka hiyo mchezaji wa Kitanzania ukisikia anaenda Uarabuni ujue huyo ni staa kwelikweli, basi Issa alibahatika kwenda Umangani, na aliporejea nchini alijiunga tena na Yanga.

Nakumbuka kipindi hicho Yanga ilikuwa na nyota kama Steven Nemes, Seleman Mkati, Kenneth Mkapa, Godwin Aswile, Salum Kabunda, Abubakar Salum "Sure Boy" Justin Mtekele, Said Mwamba, Edibili Lunyamila, Mohamed Hussein "Mmachinga" na wengineo.

Kitu cha kukumbuka kwa Issa Athuman ambaye mdogo wake ni Kassongo Athuman alikuwa anaichezea Simba, siku moja Simba na Yanga ziliumana uwanja wa Taifa wakati ule na sasa ni Uhuru, wachezaji hao wawili kila mmoja alichezea timu yake.

Basi bwana beki wa Yanga enzi hizo Salum Kabunda "Ninja" aliyesifika vibaya kwa kucheza rafu, alimrukia kifuani na miguu yote miwili beki wa Simba Kassongo Athuman ambaye alikuwa na desturi ya kupandisha mbele mashambulizi.

Ninja alitaka kumuua kabisa Kassongo kwani ilibidi awahishwe Muhimbili kufuatia rafu mbaya aliyochezewa na Ninja ambaye kwa sasa naye ni marehemu, baada ya Kassongo kuumizwa vibaya, Issa Athuman siku ile alikuwa nahodha wa Yanga alikasirishwa na rafu ya Ninja na kumfuata kwa karibu akitaka kumchapa.

Hapo ndipo ikaibuka songombingo kati ya Issa wa Yanga na Ninja pia wa Yanga, kweli damu nzito kuliko maji, Issa ameipa Yanga mataji kadhaa likiwemo kombe la Kagame

Kikosi cha Yanga kilichotwaa klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Kampala, Uganda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA