Yanga yaifuata kibabe Township Rollers
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga Sc wameondoka alfajiri ya leo kuelekea Gabolone Botswana kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Township Rollers wiki hii.
Mabingwa hao wanekwea pipa alfajiri ya saa 10:00 na nyota wake 20, Yanga inahitaji ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili kuingia hatua ya makundi ama sivyo itaondolewa mashindanoni.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam juma lililopita, Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-1 na kujiweka katika mazingira magumu, lakini mabingwa hao wa Bara wameenda Botswana wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuichapa Stand United mabao 3-1 na kufanikiwa kuwakamata mahasimu wao kileleni Simba Sc wenye pointi 46 na sasa timu hizo zinazidiana mabao ya kufunga tu