HATIMAYE DONALD NGOMA FITI KUZIVAA SINGIDA, DICHA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Daktari mkuu wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Edward Bavu amemwashia taa ya kijani mshambuliaji hatari wa mabingwa hao nchini, Mzimbabwe, Donald Ngoma kurejea uwanjani na kucheza dhidi ya Singida United Aprili 1 na Welayta Dicha Aprili 8 kwakuwa yuko fiti kwa asilimia 89.
Ngoma alikuwa majeruhi kwa muda mrefu tangia mzunguko wa kwanza lakini ni habari njema kabisa kwa mabingwa hao wa bara ambao wana mtihani mzito kusonga mbele katika mechi zake za mashindano.
Mbali na kurejea kwa Donald Ngoma ambaye anasifika kwa upachikaji mabao, Mrundi, Amissi Tambwe naye amerejea uwanjani hivyo sasa kunawafanya Wanayanga kutuliza mioyo yao kwani mastaa wao wote sasa wamerejea baada ya hivi karibuni Mzimbabwe Thabani Kamusoko kurejea