DOGO JANJA AWEKWA MTEGONI NA MKEWE
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Hatimaye msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Dogo Janja amejikuta akiwekwa mtegoni na mke wake Irene Uwoya ambaye ni staa pia wa tasnia ya filamu nchini.
Wawili hao walifunga ndoa yapata miezi mitano iliyopita na mpaka sasa ndoa yao imefikia patamu ambapo kila mmoja amekuwa akimwonea wivu mwenziye.
Lakini kwa Dogo Janja mambo yamekuwa magumu hasa baada ya kuzuiwa na mkewe kujihusisha na wanawake wengine ikiwemo hata kuwashirikisha kwenye video yake ya wimbo mpya Wayu wayu.
Katika video hiyo, Dogo Janja imemlazimu kushiriki kama mwanamke hasa baada ya kutakiwa asimshirikishe mwanamke mwingine, kuhusu upendo, Dogo Janja alipoulizwa na chombo kimoja cha habari alisema anampenda mkewe kwa asilimia 100 wakati Uwoya alipoulizwa naye akasema anampenda Janjaro kwa asilimia 80