Simba yaiendea Njombe Mji, Iringa, kuwakosa Mkude, Bocco na Fabregas
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba Sc kesho Jumamosi wanatarajia kuelekea mkoani Iringa tayari kabisa kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mji Njombe Fc uwanja wa Sabasaba, Njombe Jumanne ya Aprili 3 mwaka huu.
Vinara hao watakaa mjini Iringa hadi Jumatatu ambapo wataelekea Njombe, Simba itawakosa wachezaji wake wanne ambao ni majeruhi.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kikosi kitasafiri kesho kuelekea Iringa kabla ya kuifuata Njombe Mji, Jumatatu ambapo siku moja wataumana.
Manara amesema Simba itamkosa kiungo wake Jonas Mkude ambaye aliumia kifundo cha mguu, pia itamkosa nahodha wake John Raphael Bocco ambaye aliumia, pia itaendelea kuwakosa Haruna Niyonzima na Salim Mbonde, Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 46 na hiyo ni mechi ya kiporo