Steve Barker aihofia safu ya ushambuliaji Geita
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kinakabiliwa na changamoto ya kuwakosa wachezaji kadhaa katika mchezo unaofuata dhidi ya Geita Gold, huku akiahidi kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya ushindani huo.
Barker ameeleza kuwa kuna idadi kubwa ya wachezaji wanaoweza kukosa mchezo huo kuliko inavyofikiriwa, kutokana na adhabu na majeraha mbalimbali.
Amesisitiza kuwa kukosekana kwa wachezaji hao ni sehemu ya mchezo na benchi la ufundi linaendelea kujiandaa vyema ili kuwa tayari kukabiliana na Geita Gold.
Akizungumzia wapinzani wao, kocha huyo amekiri kuwa Geita Gold ni timu nzuri, iliyofundishwa vyema na inayojua kufunga mabao, hivyo anatarajia mchezo mgumu wenye ushindani wa hali ya juu.
