Mbwana Samatta afunga bao la msimu
Nahodha wa zamani wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefungua akaunti yake ya magoli kwenye Ligi Ligi kuu Ufaransa (Ligue 1) na kuisaidia timu yake ya Le Havre kuondoka na alama moja kwenye sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Olympique Lyon.
Le Hevre walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Nahodha wa zamani wa Tanzania, Mbwana Samatta dakika ya 74 kabla ya Lois Openda kuisawazishia Lyon dakika ya 87 na kufanya timu hizo kugawana alama moja
