Wachezaji 15 Afrika wanaolipwa zaidi, Girumugisha ashika ya 3
Jean Claude Girumugisha amekuwa mchezaji wa tatu anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya soka barani Afrika, ikiwa tunazingatia mishahara inayolipwa katika mashindano ya ndani ya Afrika pekee.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Story Africa, hawa ndio wachezaji wanaodaiwa kulipwa mishahara mikubwa zaidi katika historia ya soka la ndani barani Afrika:
1. Fiston Mayele — analipwa dola milioni 5 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli.
2. Mohamed Tougai — analipwa dola milioni 3.7 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli.
3. Jean Claude Girumugisha — analipwa dola milioni 2.4 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli .
4. Ferjani Sassi — aliwahi kulipwa dola milioni 2.2 kwa mwaka na Zamalek kati ya 2018 na 2021.
5. Ali Maaloul — aliwahi kulipwa dola milioni 1.5 kwa mwaka na Al Ahly kati ya 2021 na 2025.
6. Anthony Modeste — aliwahi kulipwa dola milioni 1.5 kwa mwaka na Al Ahly kati ya 2023 na 2024.
7. Ramadan Sobhi — analipwa dola milioni 1.446 kwa mwaka na Pyramids FC tangu 2020.
8. Youcef Belaïli — aliwahi kulipwa takribani dola milioni 1.436 kwa mwaka na MC Alger kati ya 2023 na 2024.
9. Achraf Bencharki — aliwahi kulipwa dola milioni 1.4 kwa mwaka na Zamalek kati ya 2019 na 2022.
10. Lamine Camara — analipwa dola milioni 1.2 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli .
11. Percy Tau — aliwahi kulipwa dola milioni 1.2 kwa mwaka na Al Ahly kati ya 2021 na 2025.
12. Badr Benoun — aliwahi kulipwa dola milioni 1 kwa mwaka na Al Ahly kati ya 2020 na 2022.
13. Ahmed Fathi — aliwahi kulipwa dola milioni 1 kwa mwaka na Pyramids FC kati ya 2020 na 2024.
14. Mohamed Awad — analipwa dola milioni 1 kwa mwaka na Zamalek tangu 2019.
15. Hussein El Shahat — analipwa dola milioni 1 kwa mwaka na Al Ahly tangu 2019.
Al Ahli Tripoli ya Libya inaonekana kuwa klabu inayotawala kwenye orodha hiyo, ikiwa na wachezaji kadhaa wanaolipwa mishahara mikubwa.
