Yanga yazidi kupaa kileleni
Young Africans maarufu Yanga SC yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Mchezo huo wa Ligi Kuu bara, Yanga iliandika mabao hayo kupitia kwa Peter Shalulile na Mudathir Yahya, kwa matokeo hayo Yanga insfikisha pointi 15 ikiwa imecheza mechi 5 na imefunga mabao 15.
