Djuma Shabani: Beki wa kulia aliyepita Young Africans
Djuma Shabani, alizaliwa Machi 16, 1993 huko Kindu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ni mwanasoka wa kulipwa kutoka DR Congo anayecheza nafasi ya beki wa kulia.
Djuma ni moja ya Wachezaji wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba, kupandisha mashambulizi, na kupiga penalti.
Djuma alianza soka lake la ushindani katika klabu mbalimbali nchini mwake DRC kabla ya kusajiliwa na FC Renaissance du Congo ambapo alikuwa nahodha na nguzo muhimu ya ukuta. Baadaye alihamia klabu kubwa ya AS Vita Club mwaka 2017.
Akiwa na AS Vita Club Djuma alipata mafanikio makubwa yakiwemo Kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya DRC (Linafoot) msimu wa 2017–18, Kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup) mwaka 2018 kabla ya kupoteza mbele ya Raja Casablanca ya Morocco.
Juni 2021, Djuma Shabani alihamia rasmi nchini Tanzania na kusaini mkataba na klabu ya Young Africans . Katika kipindi chake akiwa Yanga, alijinyakulia upendo mkubwa kutoka kwa mashabiki kutokana na
Uwezo wake uwanjani, Utulivu wake akiwa uwanjani, uwezo wa kuzuia washambuliaji wa pembeni, na jinsi alivyokuwa akitumika kupiga penalti kwa ustadi.
Djuma Alichangia kwa kiasi kikubwa Yanga kutwaa mataji mfululizo ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho (ASFC), na Ngao ya Jamii.
Baada ya kuondoka Yanga, Djuma Shabani amecheza katika vilabu vingine vikiwemo Namungo FC ya Tanzania kisha kurejea AS Vita Club.
Kwenye timu ya taifa ya DR Congo (Leopards), Djuma amewahi kuitwa na kucheza mechi za michuano ya kimataifa mwaka 2019 wakati wa kuwania tiketi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Djuma anakumbukwa na mashabiki wengi wa soka la Bongo kama mmoja wa mabeki bora wa kulia wa kigeni waliowahi kucheza kwa kiwango cha juu na kuacha alama ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania.

