Singida BS yaishushia lundo la magoli Polisi Tanzania
Timu ya Singida BS usiku huu imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Polisi Tanzania katika uwanja wa Airtel uliopo mjini Singida mchezo wa Ligi Kuu bara.
Ilianza Polisi kupitia Baraka Michael na goli lao la pili lilifungwa na Ibrahim Ame.
Wenyeji Singida BS wakafungua karamu ya magoli kupitia Jonathan Sowah, kisha James Mwashinga, Shekhan Ibrahim na baadae Jeancy Mboma akaweka goli la nne.
