Said Mtanda aisifu Pamba Jiji kufungwa 2-0 na Yanga
Licha ya Pamba Jiji FC kupokea kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa jana, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mlezi wa klabu hiyo, Said Mtanda— ambaye pia ni shabiki wa damu wa klabu ya Yanga SC ameeleza kuridhishwa kwake na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo.
Mtanda ameeleza kuwa watu wengi walidhani Pamba Jiji ni timu dhaifu na ingekubali kipigo kizito cha magoli matano (5) au zaidi kutoka kwa Yanga SC, lakini wameonyesha ushindani mkubwa uwanjani.
Kilichomfurahisha zaidi ni uamuzi wa kocha kuwatumia wachezaji sita (6) kutoka kikosi cha vijana cha U-20 kwenye mchezo huo dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga.
Mtanda ametoa kauli hizo baada ya kushuhudia mchezo wake wa mwisho kabla ya kuondoka Mwanza, na kuelekea Mkoa wa Simiyu kuendelea na majukumu yake.
