Nabi ajiuzuru

Kocha Nasreddine Mohammed Nabi, rasmi amejiuzulu nafasi yake ya kocha mkuu ndani ya Raja CA baada ya kinachosemwa kutofautiana na mkurugenzi wa michezo "sporting director" wa klabu hiyo.

Moja ya makubaliano ambayo Nabi alitilia mkazo wakati anasaini mkataba ni pamoja na kuhusishwa kwenye usajil wa wachezaji wapya ikiwemo matakwa yake yeye na moja ya wachezaji aliowakosa na kupelekea mzozo ni Thapelo Maseko ambaye ametimkia Copenhagen Nabi alikua anamtaka huku Sporting Director anasema hafai kwenye mpango wa klabu

Nabi amehudumu ndani ya Raja CA kwa muda wa miezi 2 na nusu sawa na siku 78 tu tangu alipoteuliwa June 12, 2026 Kwasasa Nabi yuko zake huko Brussels, Ubelgiji kupumzika lakini kusikilizia majibu ya uongozi wa Raja CA kuhusu barua yake


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI