Allasane Kante atemwa Simba

Jioni ya leo Klabu ya Simba imemuaga kiungo wake Allasane Kante, katika mchakato wa maboresho na mabadiliko ndani ya kikosi cha Mnyama.

Lakini binafsi, niliona bado Kante alikuwa na nafasi pale Msimbazi. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaba, kushinda mipira na kuanzisha mashambulizi, hasa kupitia pasi zake zenye ubora.

Wakati mwingine kwenye maboresho ya kikosi, si kila anayeondoka alikuwa hafai. Kante alikuwa na kitu chake ndani ya uwanja.

Huenda Simba wameona kitu kingine mbele, lakini kwangu mimi, kumuacha Kante ni uamuzi ambao bado utahitaji kuthibitishwa na matokeo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI