CAF yazitaka klabu shiriki mashindano yake kuandaa bajeti

CAF imeziomba klabu 115 zinazoshiriki CAFCL na CAFCC kuandaa bajeti stahiki za kina za gharama za usafiri kwa msimu mpya wa 2026-27 na kuziwasilisha kwa shirikisho hilo.

Mkutano huo ulifanyika Jumapili hii iliyopita na kuongozwa na Mwenyekiti wa ACA na Rais wa Young Africans SC Eng Hersi Said ili kupunguza gharama za vifaa na fedha.

Eng Hersi Said alihakikisha kuwa Rais wa CAF Patrice Motsepe amejitolea kutafuta suluhisho la changamoto hizo na lengo kuu ni kurahisisha usafiri, kupunguza gharama zisizo za lazima na kuboresha hali za klabu katika mashindano hayo ya kimataifa.

Mkutano huo uliandaliwa na ACA kwa lengo la kutafuta suluhisho la Ugumu wa Usafiri katika mashindano ya Bara.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI