Geita Gold yaifuata Simba na ndege
Kikosi cha Geita Gold FC kimewasili rasmi jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa ndege ya Air Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao miwili mikubwa ya NBC Premier League dhidi ya miamba ya soka nchini, Simba SC na Yanga SC.
Hii ni mara ya pili msimu huu kwa Geita Gold kutumia usafiri wa anga kusafiri kuelekea mechi zao ili kuwapa wachezaji mapumziko ya kutosha na kuepuka athari za safari ndefu za barabarani.
