Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2023

PITSO MOSIMANE AFUTWA KAZI

Picha
Uongozi wa klabu ya Al Wahda umemfuta kazi kocha wake mkuu, Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini kufuatia mwenendo usioridhisha wa matokeo katika klabu hiyo iliyopo ligi kuu ya Falme za Kiarabu (UAE). Hapo jana klabu hiyo ilipokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Shabab Al Ahli Klabu ya Al Wahda sasa inakamata nafasi ya 6 ikiwa na alama 9 latika ligi kuu nchini humo.

CAF AWARDS 2023 SASA NI DESEMBA 11

Picha
Baada ya juzi kushuhudia usiku wa Ballon d'Or sasa ni muda wa Tuzo za Wachezaji wa Soka Barani Afrika, kupitia ukurasa wa Instagram. Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeutangaza usiku wa Desemba 11, 2023 kuwa ndiyo utakuwa maalumu kuwapa tuzo waliofanya vyema kwenye soka mwaka huu.

IBRAHIM BAKA AREJEA KMKM

Picha
Beki kisiki wa timu ya taifa Tanzania (Taifa Stars) na timu ya taifa ya Zanzibar na klabuya Young Africans SC Ibrahim Baka akiwa na wachezaji pamoja na viongozi wa tumu yake ya zamani KMKM SC mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya KVZ FC, ambaouliomalizika kwa KMKM kuwafungo KVZ 2-0 huku KMKM ikiwa pungufu. Baka aliamua kuwatembelea KMKM timu ambayo ilimtoa kisoka kabla ya kutua Yanga, mchezaji huyo atashiriki kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba utakaofanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam

HATMA YA MOSES PHIRI KUBAKI SIMBA WIKI IJAYO

Picha
Makubaliano kati ya klabu ya Simba na Menejiment ya Mshambuliaji Moses Phiri yatafanyika mwanzoni mwa wiki ijayo ili kumuongezea mchezaji huyo mkataba mpya. Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Moses Phiri anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru (Free agent) ambapo kadhaa zinahitaji kuipata saini yake. Kuna baadhi ya timu zinahitaji kuipata saini ya Moses Phiri, za Kaskazini zinatarajia kutuma ofa hivi karibuni kwa Menejiment ya Mchezaji huyo huku za Mashariki zinatarajia kumpa kishika uchumba mwezi ujao. Taarifa za uhakika kwa mujibu wa vyanzo vyangu ni kuwa Moses Phiri ameipa kipaumbele kikubwa zaidi Simba kuanzia ofa yao na vipengele vingine vya kimkataba ijapo hajasaini karatasi zozote mpaka sasa. Simba wanapambana sana kukamilisha dili la kumuongezea Moses Phiri mkataba mpya kwa wakati.

MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

Picha
Wachezaji Mudathir Yahya wa Yanga na Feisal Salum wa Azam watafungiwa michezo mitatu kila mmoja na faini isiyopungua laki tano (500,000/-) kwa kosa la kukwepa kupeana mikono na waamuzi na timu pinzani adhabu hiyo kwa uvunjifu wa kanuni ya 41(5) (5.4) ya ligi kuu ya NBC kuhusu udhibiti wa wachezaji. Mudathir na Feisal hawakupeana mikono na waamuzi na wachezaji wa timu pinzani kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Azam wachezaji hao walikuwa nje ya mstari (touch line) wakitegeana kuingia uwanjani mpaka zoezi la kupeana mikono kwa timu na waamuzi kuisha ndio wakaingia uwanjani. Iwapo kamati ya masaa 72 itatoa adhabu yake kabla ya michezo ya raundi ya 7 wachezaji hao watakosa michezo ifuatayo Mudathir (Singida, Simba, Coastal), Feisal (Namungo, Mashujaa na Ihefu) iwapo adhabu itatoka baada ya michezo ya raundi ya 7 watakosa michezo ifuatayo Mudathir (Simba, Coastal, Mashujaa), Feisal (Mashujaa, Ihefu Mtibwa).

HAJI MANARA AITABIRIA USHINDI YANGA DHIDI YA SIMBA

Picha
"Haijawahi kuwa mechi rahisi zinapocheza Yanga na Simba, na kutabiri matokeo unaweza kiuchawi au kibeting, ila kujua matokeo halisi haiwezekani, huwezi jua nani atashinda au kufungwa hata kama team moja ipo katika mazingira rafiki zaidi ya kushinda hiyo mechi. Pamoja na hayo karata yangu nawapa nafasi kubwa ya @yangasc kushinda kwa sababu za kiufundi zaidi, ili Yanga wafungwe itabidi wafanye makosa mengi mno katika defence line yao, otherwise ule utatu wa @maxinzengeli, @pacom_zouzoua na @aziz.ki.10 unakwenda kumaliza mechi mapema".

PIUS MPENDA ADUNDA MTU UTURUKI

Picha
Bondia Mtanzania Pius Mpenda ameshinda ubingwa wa 'WBC Peace Champion' usiku wa kuamkia leo katika pambano lililopigwa Jijini Istanbul Uturuki. Mpenda ameshinda pambano hilo dhidi ya Dauren Yeleussionov raia wa Kazakhstan kwa pointi za majaji wote. Huu ni ushindi wa tatu kwa Mpenda katika kipindi cha miaka 11 huku akitwaa ubingwa mara mbili.

SIMBA IMEPAMBANA ILA BAHATI HAIKUWA YAO

Picha
BAHATI haikuwa yao Wekundu wa Msimbazi, Simba SC dhidi ya Al Ahly Jumanne iliyopita mchezo wa marudiano uliofanyika jijini Cairo.  Katika mchezo huo wa michuano ya African Football League, timu hizo zilifungana mabao 1-1 na kufanya ziwe zimefungana kwa jumla ya mabao 3-3, katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Mkapa timu hizo zenye ushindani wa aina yake zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2.  Sare ya jijini Dar es Salaam iliwafanya Simba kuaga michuano hiyo licha kwamba zilitoka sare tena jijini Cairo, magoli mawili ya ugenini yaliipa faida Ahly na kusonga mbele.  Al Ahly sasa itakutana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini hatua ya nusu fainali, Ahly ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika. Na pia ni mabingwa watetesi wa Ligi ya mabingwa Afrika, uwezo mkubwa ilionao sidhani kama timu nyingine inayoweza kukabiliana nayo kwani imekuwa ikizitesa timu inazokutana nazo.  Ingawa imekuwa ikikutana na upinzani mkali hasa na timu nyingine za kiarabu kutoka Afrik...

SIMBA ITAENDELEA KUMFUNGA YANGA- AHMED ALLY

Picha
Meneja Habari wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema ni kawaida yao Simba kuendeleza ushindi mbele ya. Watani wao wa jadi Yanga SC siku ya Jumapili watakapokutana. "Ni mechi ambayo tunakwenda kuendeleza ubabe kwa watani zetu. Ili tujiridhishe kwamba msimu huu tutafanya vizuri ni kupata ushindi katika mchezo huo. Tunataka tuchukue ubingwa mapema sana, katika hili tunawashukuru Ihefu kwa kutusaidia kazi na sisi tunataka kuendeleza kuweka tofauti ya alama na Yanga SC

YANGA KUISHITAKI SIMBA TFF

Picha
-Mkurugenzi wa sheria wa Yanga amesema kesho klabu ya Yanga itawasilisha rasmi malalamiko yake kwenye mamlaka juu ya kitendo cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga. "Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisa, hakuna sababu ya msingi kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni Watani wa jadi sio maadui" "Isije kufika siku hatuwezi kukaa kwa pamoja kama ndugu kwa sababu ya UPUMBAVU kama huu" "Naiomba bodi ya ligi @tplboard, TFF @tanfootball na Polisi @policetanzania wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe" "Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama" "Shame on you all who're involved in this incident" "Mwenye kumjua na kuwa na mawasiliano ya huyu (Shabiki wa Yanga aliyepigwa na mashabiki wa Simba) anitumie tafadhari"

ROBERTINHO ASEMA SIMBA ITAOGOPWA NA VIGOGO AFRIKA

Picha
Kocha wa Klabu ya soka ya Simba, Roberto Oliviera 'Robertinho', amesema umefika wakati sasa kwa timu barani Afrika kuanza kuogopa kucheza na timu yake. Robertinho ameyasema hayo baada ya timu yake kuivimbia Al Ahly ya Misri na kutolewa kwa sheria ya bao la ugenini huku zikifungana mabao 3-3. Kocha huyo amesema imefika wakati sasa timu yake ya Simba itaogopwa na vigogo barani Afrika kwani ikifikia timu imepangwa na Simba itaanza kujiuliza mara mbili mbili

MO DEWJI ATEUA WAJUMBE WA BODI YA BARAZA LA USHAURI SIMBA SC

Picha
Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Ushauri la Simba Sports Club Company Limited ambao wameteuliwa na Rais wa heshima, Mohammed Dewji.

MTANZANIA APIGA BONGE LA GOLI SERBIA

Picha
Beki wa Kimataifa wa Tanzania Alphonce Mabula hapo jana alifunga goal moja wakati klabu yake ya Fk Novi Sad ikipoteza mchezo kwa mabao 2-1 dhidi ya Sloboda katika mchezo wa ligi Daraja la kwanza nchini Serbia. Hili ni bao lake la 2 katika michezo minne aliyocheza tangu ajiunge klabuni hapo. Mabula anacheza Ligi moja na Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Simba,Dejan Georgejivc

TETESI, LAVALAVA KUONDOKA WCB

Picha
Kwa mujibu wa watu wakaribu wa Msani wa Muziki wa Bongo fleva Lava lava Tayari Ameshavunja mkataba na lebo yake ilikuwa ikimsimamia ili kuanza kujitegemea Akiwa Kama Solo Artist kilichobaki kwa Sasa Ni kukamilisha malipo ya uvunjaji mkataba ambapo kwa Sasa wameshalipa Asilimia kadhaa na wanategemea kukamilisha malipo yaliyobaki ili kukabidhiwa hatimiliki za digital platform zake na Mambo mengine .kumbuka hii sio Mara ya kwanza kwa wasani kutoka Wcb kuvunja mikataba hii imefanyika kwa Rich mavoko, Harmonize, Rayvanny Sasa Ni lavalava

MIQUISSONE AGEUKA LULU SIMBA

Picha
Luis Miquissone ni silaha ya maangamizi pale Msimbazi Hadi sasa . Nyota huyu ndani ya mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu ya NBC amechangia alama Sita Kwa Kikosi chake Cha @simbasctanzania . Aliingia toka benchi katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate akatoa Assist Kwa Moses Phiri aliyefunga bao la ushindi. Katika mchezo dhidi ya Ihefu ameingia kutoka benchi ametoa Assist Kwa Moses Phiri Ambaye bila Ajiz akaweka Mpira nyavuni. Mechi mbili zilizopita za Ligi Simba wamevuna alama (6) Kwa mchango mkubwa wa Luis Miquissone.

PHIRI ATUMA SALAMU KWA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr Bao lililofungwa na mshambuliaji Moses Phiri dqkika ya 65 limeiwezesha Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ijefu SC ya Mbeya katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara. Kwa matokeo hayo bado Simba inaendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya Yänga lakini ikiwa na pointi 18 sawa na Yanga isipokuwa wanazidiwa magoli ya kufunga. Simba ilianza kufunga bao la kwanza likiwekwa kimiani na Jean Baleke dakika ya 13 kabla ya Ihefu SC kusawazisha kupitia Ismail Mgunda dakika ya 25 kabla ya Phiri kufunga la ushindi.

NAMUNGO YAPELEKA MSIBA CHAMAZI

Picha
Bado hali si shwari kwa wanalamba lamba wa mitaa ya Chamazi, Azam FC baada ya usiku huu kupokea kichapo cha mabao 3-1 toka kwa Namungo FC ya Ruangwa katika mfululizo wa Ligi Kuu bara. Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwani mapema tu ilitoka kufungwa mabao 3-2 na Yanga SC, mabao ya Namungo yamefungwa na Pius Buswita dakika ya 10, Hashim Manyanya dakika ya 19 na Reliants Lusajo dakika ya 49, goli pekee la Azam limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70

DJUMA SHABANI KUONDOKA NA WAWILI AZAM FC

Picha
Dirisha dogo la usajili klabu ya Azam itaachana na wachezaji wake wawili (Majina kapuni) ili kupisha maingizo mapya kikosini hapo. Ingizo la kwanza ni la Djuma Shaaban raia wa Congo DRC ambaye tayari anafanya mazoezi na nyota wengine wa Azam. Aidha Mlinda mlango wa Tabora United John Noble raia wa Nigeria ambaye alijiunga na nyuki akitokea Enyimba ya Nigeria anatajwa huenda akajiunga na Azam dirisha dogo la usajili kama mipango itaenda sawa.

STARS YAZINDUA JEZI ZAKE MPYA

Picha
Shirikisho la Soka nchini (TFF), limetambulisha jezi mpya zitakazotumika na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). . Jezi hizo za aina tatu, ambayo ya nyumbani (Home kit) yenye rangi ya bluu, ya ugenini (Away Kit) yenye rangi ya njano na bluu, pamoja na jezi ya tatu (Third Kit) yenye rangi nyeusi na kijani.

MAYELE AENDELEA KUTETEMA MISRI

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC Fiston Mayele raia wa DR Congo ameendelea kutetema akiwa na klabu yake mya ya Pyramids baada ya kuifungia mabao mawili timu hiyo katika ushindi wa mabao 4-2 mchezo wa Ligi Kuu ya Misri. Mayele akiyefunga mabao hayo daiika ya 45 na 85 huku mabao mengine yalifungwa na Shami katika dakika ya 48 na Fathi dakika ya 85

YANGA YAICHAKAZA SINGIDA FOUNTAIN GATE 2-0

Picha
Mabao mawili yaliyofungwa na kiungo mshambuliaji Maxi Mpia Zengeli usiku wa leo yameiwezesha timu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu bara uliofanyika kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Maxi raia wa DR Congo alifunga mabao yote kipindi cha kwanza na kuifanya timu yake iendelee kukaa kileleni ikiwa na alama 18 ikiwa imecheza mechi 7 huku ikifuatiwa na hasimu wake Simba SC ambao kesho watakutana na Ihefu SC kwenye uwanja huo huo. Wakati huo mchezo mwingine wa ligi hiyo unaendelea kati ya Azam FC na Namungo FC ambapo hadi tunaenda mitamboni Namungo ilikuwa inaongoza kwa mabao 3-1

MKUDE AMSHITAKI MO DEWJI, ADAI BIL 1

Picha
Kiungo wa Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 Bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter bila idhini yake.

BEKI YANGA AIOTA UFARANSA

Picha
Beki wa kati wa Yanga aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu, Gift Fred amefunguka kwamba ana ndoto inayomtamanisha kwenda Ufaransa ili kupata urahisi wa kuonwa na timu nyingine kubwa zaidi Ulaya. . “Kama ikitokea nafasi hiyo, Ligi ya Ufaransa nadhani ndio sehemu nzuri zaidi kwenda kucheza kwa sababu inavyooneka timu nyingi zinaangalia kule, lakini pia hata wachezaji wa Ufaransa wanaonyesha wanapigiana chapuo pindi wanapoenda kwingine. . “Ndoto ya kucheza soka la kulipwa Ulaya bado ipo kwani bado nina umri sahihi na naamini nina kipaji cha kunifikisha huko.” alisisitiza beki huyo. . Tangu alipojiunga na Yanga, beki huyo bado hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kocha Miguel Gamondi

MAPOKEZI YA MAKONDA YAFUNIKA

Picha
Mapokezi ya katibu mwenezi mpya wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Paul Makonda umezua balaa kwani idadi kubwa ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi. Makonda alipokelewa ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo pia aliweza kuzungumza. "Niseme tu kuanzia leo Oktoba 26, 2023, Taifa hili halina chama cha upinzani bali lina vyama vya watoa taarifa, na sisi kama chama tawala tutafanyia kazi taarifa zao kwa sababu ni chachu ya ujenzi si tu wa demokrasia bali wa maendeleo katika Taifa letu,"- Paul Makonda, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

WIMBO WA DIAMOND WAZUA BALAA MAREKANI

Picha
Wimbo wa Diamond Platnumz #shu unasikizwa sana Marekani, kwa mujibu wa Roma Mkatoliki ameandika kupitia InstaStory yake wimbo unapigwa sana Jijini Washington DC, Marekani. Roma ameandika hayo kupitia Instastory yake... "Kibane baaane mwisho kiliwe na nyenyere huu muwa unalia sana DC club nyingii!!!"

BRUNO GOMES KUAMKIA KWA YANGA KESHO?

Picha
Bruno Gomes hawiki sana msimu huu ndani ya Ligi Kuu ya NBC baada ya kubadilishiwa majukumu ndani ya Dimba . Nyota huyu Kwa sasa anasimama nyuma ya Marouf Tchakei,Duke Abuya na nyota wengine wengi ambao wapo kwenye Kikosi Cha Singida Fountain Gate . Hiii inamfanya asiwe karibu na lango la mpinzani ndiyo maana hatushuhudii akicheka na nyavu kama ambavyo alikuwa anafanya msimu uliopita. Huyu ni Moja ya Viungo wa kati bora ndani ya Ligi yetu Bruno Baroso ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi zenye macho ....iwe long pass or Short Pass Katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo, alisimama nyuma ya Duke Abuya, Tchakei, Habib/Kazadi na Kaseke wakati Singida Fountain Gate wakiwadunda Namungo 3-2 pale Ruangwa. Kesho Singida Fountain Gate itakutana na Yanga katika uwanja wa Mkapa, Gomes anatarajia kuonyesha mchezo mzuri ama kushindwa kufurukuta

WCB KUTAMBULISHA MSANII MPYA

Picha
Records Label ya WCB Wasafi ipo mbioni kumtambulisha msanii mpya ambaye ana kipaji kikubwa, hiyo ni kwa mujibu wa Diamond Platnumz. "Licha ya ukubwa wa Project zote zilizo ndani Wasafi, ila kiukweli moja ya Project ambayo niko nayo very excited ni kumtambulisha huyu Msanii mpya wa Wasafi, itoshe kusema Tanzania ina vipaji." ameandika Diamond X.

YANGA YAIEKEA KIKAO KIZITO SIMBA

Picha
Kamati ya Utendaji Young Africans SC chini ya Rais wetu Hersi Ally Said leo tarehe 25.10.2023 wamekaa kikao cha pili cha kikatiba kwa mwaka 2023 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuzungumzia mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa Klabu yetu.

MTANZANIA KUWANIA UBINGWA WA WBC UTURUKI

Picha
Bondia Pius Mpenda a.k.a 'Super Hero' kutoka Naccoz gym chini ya kocha wake Rama Jah tarehe 29/10/2023 anatarajiwa kupanda ulingoni kwenye pambano la kimataifa nchini Uturuki. Wastani wa Mpenda kwenye mapambano yake ya kimataifa nnje ya mipaka ya Tanzania umekuwa mzuri amecheza jumla ya mapambano matatu ya kimataifa ameshinda mawili na kupoteza moja na amefanikiwa kutwaa mkanda mmoja wa dunia wa WBU. Mpenda atacheza na bondia Dauren Yeleussinov mzaliwa wa jiji la Kayindy nchini Kazakhstan ila ni mkazi wa jiji la Brooklyn, New York nchini Marekani. Mpenda na Yeleussinov watacheza pambano la raundi 10 ubingwa wa WBC (World Boxing Council Peace Super Welterweight kg 69 title) litakalo fanyika kwenye ukumbi wa Hilton Double jijini Instanbul nchini Uturuki. Mpinzani wake Mpenda bondia Yeleussinov alianza safari yake ya mchezo wa masumbwii kupitia ngumi za Amateur (Ngumi za Ridhaa) tarehe 17/12/2005 dhidi ya bondia Ruslan Safiullin raia wa Kazakhstan kwenye pambano la raundi 4 na bon...

BEKI LIVERPOOL ASHIKANA MASHATI NA KOCHA WAKE

Picha
Unaambiwa mlinzi wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho (33) ambaye kwasasa anakipiga Montpellier amegombana na kushikana mashati kocha wake Der Zakarian wakiwa mazoezini. Ripoti inaeleza kuwa katika mazoezi yaliyofanyika jana (Jumanne) jioni Sakho alisusa na kuamua kutoka nje ya uwanja wa mazoezi mara baada ya kufanyiwa madhambi na kutopewa faulo, ambapo katika chumba cha kubadilishia nguo wawili hao walianza kubishana na ndipo Kocha huyo akamzomea kwa kumwambia "Cry-Baby" ndipo Sakho alipojibu kwa kumshika kola ya shati na kumwangusha chini kocha huyo mpaka pale wachezaji wengine walipoingilia kati. Inaelezwa kuwa Sakho amekuwa kwenye wakati mgumu sana chini ya kocha huyo, ambapo msimu huu amecheza dakika 6 tu.

OSCAR MIRAMBO AULA CAF

Picha
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Oscar Mirambo ameteuliwa na CAF kuwa Mkufunzi wa Kozi ya wakufunzi wa CAF Elite (CAF Elite Instructors Course) inayofanyika Rabat, Morocco.

ADAM SALAMBA HUYOOO LIBYA

Picha
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Adam Salamba amejiunga na Club ya Libyan stadium inayo shiriki ligi Daraja la kwanza nchini Libya Akitokea Ghazil el Mahalla Ya Nchini Misri

SIMBA YAIGOMEA AHLY LAKINI YATUPWA NJE

Picha
Bao lililofungwa na kiungo mkabaji Sadio Kanoute wa Simba SC na Kahraab wa Al Ahly usiku wa leo limetosha kuzilazimisha timu hizo kufungana bao 1-1 katika mchezo wa marudiano wa michuano mipya ya African Football League mjini Cairo nchini Misri. Hiyo ni sare ya pili kwa miamba hiyo jumla zimefungana 3-3 lakini Simba inaaga michuano hiyo kwa faida ya goli la ugenini kwani katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam zilifungana 2-2, sasa Ahly itakutana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali