NAMUNGO YAPELEKA MSIBA CHAMAZI
Bado hali si shwari kwa wanalamba lamba wa mitaa ya Chamazi, Azam FC baada ya usiku huu kupokea kichapo cha mabao 3-1 toka kwa Namungo FC ya Ruangwa katika mfululizo wa Ligi Kuu bara.
Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwani mapema tu ilitoka kufungwa mabao 3-2 na Yanga SC, mabao ya Namungo yamefungwa na Pius Buswita dakika ya 10, Hashim Manyanya dakika ya 19 na Reliants Lusajo dakika ya 49, goli pekee la Azam limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70