PIUS MPENDA ADUNDA MTU UTURUKI
Bondia Mtanzania Pius Mpenda ameshinda ubingwa wa 'WBC Peace Champion' usiku wa kuamkia leo katika pambano lililopigwa Jijini Istanbul Uturuki.
Mpenda ameshinda pambano hilo dhidi ya Dauren Yeleussionov raia wa Kazakhstan kwa pointi za majaji wote.
Huu ni ushindi wa tatu kwa Mpenda katika kipindi cha miaka 11 huku akitwaa ubingwa mara mbili.