ROBERTINHO ASEMA SIMBA ITAOGOPWA NA VIGOGO AFRIKA
Kocha wa Klabu ya soka ya Simba, Roberto Oliviera 'Robertinho', amesema umefika wakati sasa kwa timu barani Afrika kuanza kuogopa kucheza na timu yake.
Robertinho ameyasema hayo baada ya timu yake kuivimbia Al Ahly ya Misri na kutolewa kwa sheria ya bao la ugenini huku zikifungana mabao 3-3.
Kocha huyo amesema imefika wakati sasa timu yake ya Simba itaogopwa na vigogo barani Afrika kwani ikifikia timu imepangwa na Simba itaanza kujiuliza mara mbili mbili