BEKI YANGA AIOTA UFARANSA
Beki wa kati wa Yanga aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu, Gift Fred amefunguka kwamba ana ndoto inayomtamanisha kwenda Ufaransa ili kupata urahisi wa kuonwa na timu nyingine kubwa zaidi Ulaya. .
“Kama ikitokea nafasi hiyo, Ligi ya Ufaransa nadhani ndio sehemu nzuri zaidi kwenda kucheza kwa sababu inavyooneka timu nyingi zinaangalia kule, lakini pia hata wachezaji wa Ufaransa wanaonyesha wanapigiana chapuo pindi wanapoenda kwingine. .
“Ndoto ya kucheza soka la kulipwa Ulaya bado ipo kwani bado nina umri sahihi na naamini nina kipaji cha kunifikisha huko.” alisisitiza beki huyo. .
Tangu alipojiunga na Yanga, beki huyo bado hajajihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kocha Miguel Gamondi