SIMBA YAIGOMEA AHLY LAKINI YATUPWA NJE
Bao lililofungwa na kiungo mkabaji Sadio Kanoute wa Simba SC na Kahraab wa Al Ahly usiku wa leo limetosha kuzilazimisha timu hizo kufungana bao 1-1 katika mchezo wa marudiano wa michuano mipya ya African Football League mjini Cairo nchini Misri.
Hiyo ni sare ya pili kwa miamba hiyo jumla zimefungana 3-3 lakini Simba inaaga michuano hiyo kwa faida ya goli la ugenini kwani katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam zilifungana 2-2, sasa Ahly itakutana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali