BRUNO GOMES KUAMKIA KWA YANGA KESHO?

Bruno Gomes hawiki sana msimu huu ndani ya Ligi Kuu ya NBC baada ya kubadilishiwa majukumu ndani ya Dimba .

Nyota huyu Kwa sasa anasimama nyuma ya Marouf Tchakei,Duke Abuya na nyota wengine wengi ambao wapo kwenye Kikosi Cha Singida Fountain Gate .

Hiii inamfanya asiwe karibu na lango la mpinzani ndiyo maana hatushuhudii akicheka na nyavu kama ambavyo alikuwa anafanya msimu uliopita.

Huyu ni Moja ya Viungo wa kati bora ndani ya Ligi yetu Bruno Baroso ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi zenye macho ....iwe long pass or Short Pass

Katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo, alisimama nyuma ya Duke Abuya, Tchakei, Habib/Kazadi na Kaseke wakati Singida Fountain Gate wakiwadunda Namungo 3-2 pale Ruangwa.

Kesho Singida Fountain Gate itakutana na Yanga katika uwanja wa Mkapa, Gomes anatarajia kuonyesha mchezo mzuri ama kushindwa kufurukuta



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA