MTANZANIA KUWANIA UBINGWA WA WBC UTURUKI

Bondia Pius Mpenda a.k.a 'Super Hero' kutoka Naccoz gym chini ya kocha wake Rama Jah tarehe 29/10/2023 anatarajiwa kupanda ulingoni kwenye pambano la kimataifa nchini Uturuki.

Wastani wa Mpenda kwenye mapambano yake ya kimataifa nnje ya mipaka ya Tanzania umekuwa mzuri amecheza jumla ya mapambano matatu ya kimataifa ameshinda mawili na kupoteza moja na amefanikiwa kutwaa mkanda mmoja wa dunia wa WBU.

Mpenda atacheza na bondia Dauren Yeleussinov mzaliwa wa jiji la Kayindy nchini Kazakhstan ila ni mkazi wa jiji la Brooklyn, New York nchini Marekani.

Mpenda na Yeleussinov watacheza pambano la raundi 10 ubingwa wa WBC (World Boxing Council Peace Super Welterweight kg 69 title) litakalo fanyika kwenye ukumbi wa Hilton Double jijini Instanbul nchini Uturuki.

Mpinzani wake Mpenda bondia Yeleussinov alianza safari yake ya mchezo wa masumbwii kupitia ngumi za Amateur (Ngumi za Ridhaa) tarehe 17/12/2005 dhidi ya bondia Ruslan Safiullin raia wa Kazakhstan kwenye pambano la raundi 4 na bondia Yeleussinov aliweza kushinda pambano hilo kwa matokeo ya point .

Mpaka anatoka kwenye ngumi za Amateur alikuwa na rekodi yakucheza jumla ya mapambano 37, kashinda 26, kwa "KO'S" 1, kapoteza 11 na sare 0.

Aliingia kwenye ngumi za Kulipwa (Professional Boxing) tarehe 3/12/2014 dhidi ya bondia Anthony Dwayne raia wa Marekani kwenye pambano la raundi 4 na bondia Yeleussinov aliweza kushinda pambano hilo kwa matokeo ya "TKO" kwenye raundi ya kwanza.

Mpaka sasa ni bondia mwenye hadhii ya nyota moja anacheza kwenye uzani wa Super Welterweight Kg 69 anashikilia nafasi ya 342 kati ya mabondia 1898 Duniani na nafasi namba 2 kati ya mabondia wa 5 wanaocheza uzito huo wa kg 69 nchini kwao Kazakhstan.

Akiwa na rekodi yakucheza jumla ya mapambano 14, Kashinda 11, Kwa "KO'S" 10, kapoteza 2 na sare 1.

Mpenda ni bondia mwenye hadhii ya nyota mbili anacheza kwenye uzani Middleweight kg 72 anashikilia nafasi ya 114 kati ya mabondia 1551 Duniani na nafasi namba 1 kati ya mabondia 28 wanaocheza uzito huo wa kg 72 hapa nyumbani Tanzania.

Akiwa na rekodi yakucheza jumla ya mapambano 8, kashinda 7, kwa "KO'S" 4, kapoteza 1 na sare 0.
Tunamtakia maandalizi mema bondia Pius Mpenda iliaweze kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA