HATMA YA MOSES PHIRI KUBAKI SIMBA WIKI IJAYO


Makubaliano kati ya klabu ya Simba na Menejiment ya Mshambuliaji Moses Phiri yatafanyika mwanzoni mwa wiki ijayo ili kumuongezea mchezaji huyo mkataba mpya.

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Moses Phiri anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na atakuwa Mchezaji huru (Free agent) ambapo kadhaa zinahitaji kuipata saini yake.

Kuna baadhi ya timu zinahitaji kuipata saini ya Moses Phiri, za Kaskazini zinatarajia kutuma ofa hivi karibuni kwa Menejiment ya Mchezaji huyo huku za Mashariki zinatarajia kumpa kishika uchumba mwezi ujao.

Taarifa za uhakika kwa mujibu wa vyanzo vyangu ni kuwa Moses Phiri ameipa kipaumbele kikubwa zaidi Simba kuanzia ofa yao na vipengele vingine vya kimkataba ijapo hajasaini karatasi zozote mpaka sasa.

Simba wanapambana sana kukamilisha dili la kumuongezea Moses Phiri mkataba mpya kwa wakati.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA