YANGA KUISHITAKI SIMBA TFF


-Mkurugenzi wa sheria wa Yanga amesema kesho klabu ya Yanga itawasilisha rasmi malalamiko yake kwenye mamlaka juu ya kitendo cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga.

"Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisa, hakuna sababu ya msingi kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni Watani wa jadi sio maadui"

"Isije kufika siku hatuwezi kukaa kwa pamoja kama ndugu kwa sababu ya UPUMBAVU kama huu"

"Naiomba bodi ya ligi @tplboard, TFF @tanfootball na Polisi @policetanzania wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe"

"Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama"

"Shame on you all who're involved in this incident"

"Mwenye kumjua na kuwa na mawasiliano ya huyu (Shabiki wa Yanga aliyepigwa na mashabiki wa Simba) anitumie tafadhari"


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA