SIMBA IMEPAMBANA ILA BAHATI HAIKUWA YAO

BAHATI haikuwa yao Wekundu wa Msimbazi, Simba SC dhidi ya Al Ahly Jumanne iliyopita mchezo wa marudiano uliofanyika jijini Cairo. 

Katika mchezo huo wa michuano ya African Football League, timu hizo zilifungana mabao 1-1 na kufanya ziwe zimefungana kwa jumla ya mabao 3-3, katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Mkapa timu hizo zenye ushindani wa aina yake zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2. 

Sare ya jijini Dar es Salaam iliwafanya Simba kuaga michuano hiyo licha kwamba zilitoka sare tena jijini Cairo, magoli mawili ya ugenini yaliipa faida Ahly na kusonga mbele. 
Al Ahly sasa itakutana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini hatua ya nusu fainali, Ahly ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika.

Na pia ni mabingwa watetesi wa Ligi ya mabingwa Afrika, uwezo mkubwa ilionao sidhani kama timu nyingine inayoweza kukabiliana nayo kwani imekuwa ikizitesa timu inazokutana nazo. 

Ingawa imekuwa ikikutana na upinzani mkali hasa na timu nyingine za kiarabu kutoka Afrika kaskazini na hivi karibuni ilifungwa bao 1-0 na timu ya USM Alger ya Algeria. 

Katika mchezo huo wa kuwania ubingwa wa Super Cup, ambao ulishirikisha mabingwa wa Ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho, zaidi ya hapo Ahly imekuwa kiboko yao na ikiendelea kuogopwa. 

Simba SC nayo ilikuwa miongoni mwa timu iliyopangiwa kukutana na Al Ahly, mashabiki wa Simba waliingiwa mchecheto walipopangiwa kucheza na Al Ahly, wakati ratiba ya michuano hiyo inapangwa na Ahly mashabiki wengi wa soka nchini waliikatia tamaa Simba. 

Ukiondoa TP Mazembe ya DR Congo ambayo ilikuwa ikiipa ushindani mkubwa, lakini sasa TP Mazembe imepungua makali yake, lakini Simba ni timu pekee Afrika mashariki kuweza kukabilia vikali na Ahly. 

Ushindani wa Simba haukuanzia katika mchezo wa kombe la African Football League, Wekundu hao wa Msimbazi walianza kuchuana vikali na Ahly kuanzia miaka ya 1985 ambapo Simba iliweza kuifunga mabao 2-1 katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wakati huo michuano hiyo ikijulikana kama Klabu bingwa Afrika. 

Lakini tena zilikutana msimu wa mwaka 2018/2019 zikicheza uwanja wa Mkapa mjini Dar es Salaam na Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, pia zilikutana tena msimu wa 2020/2021 katika uwanja huo huo wa Mkapa na Simba kushinda bao 1-0. 

Tofauti na mechi iliyopita ambayo ilikuwa ya mtoano ya michuano mipya ya African Football League, wengi walidhani Simba itapigwa magoli mengi hasa kutokana na Ahly kupania mchezo huo.

Na pia imefanya usajili kabambe ambapo miongoni mwa wachezaji bora waliosajiliwa ametoka barani ulaya kwenye timu ya Dortmund ya Ujerumani. 

Hata hivyo Simba walicheza kandanda safi na iliwafanya Ahly kumtimu kocha wake, kwani Wekundu hao waliupiga mwingi na kama si bahati kwa Ahly wangefungwa nyumbani na kutolewa kwenye mashindano, kwani Ahly walisawazisha baada ya kufungwa. 

ALAMSIKI


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA