HAJI MANARA AITABIRIA USHINDI YANGA DHIDI YA SIMBA
"Haijawahi kuwa mechi rahisi zinapocheza Yanga na Simba, na kutabiri matokeo unaweza kiuchawi au kibeting, ila kujua matokeo halisi haiwezekani, huwezi jua nani atashinda au kufungwa hata kama team moja ipo katika mazingira rafiki zaidi ya kushinda hiyo mechi.
Pamoja na hayo karata yangu nawapa nafasi kubwa ya @yangasc kushinda kwa sababu za kiufundi zaidi, ili Yanga wafungwe itabidi wafanye makosa mengi mno katika defence line yao, otherwise ule utatu wa @maxinzengeli, @pacom_zouzoua na @aziz.ki.10 unakwenda kumaliza mechi mapema".