MUDATHIR KUIKOSA SIMBA

Wachezaji Mudathir Yahya wa Yanga na Feisal Salum wa Azam watafungiwa michezo mitatu kila mmoja na faini isiyopungua laki tano (500,000/-) kwa kosa la kukwepa kupeana mikono na waamuzi na timu pinzani adhabu hiyo kwa uvunjifu wa kanuni ya 41(5) (5.4) ya ligi kuu ya NBC kuhusu udhibiti wa wachezaji.

Mudathir na Feisal hawakupeana mikono na waamuzi na wachezaji wa timu pinzani kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Azam wachezaji hao walikuwa nje ya mstari (touch line) wakitegeana kuingia uwanjani mpaka zoezi la kupeana mikono kwa timu na waamuzi kuisha ndio wakaingia uwanjani.

Iwapo kamati ya masaa 72 itatoa adhabu yake kabla ya michezo ya raundi ya 7 wachezaji hao watakosa michezo ifuatayo Mudathir (Singida, Simba, Coastal), Feisal (Namungo, Mashujaa na Ihefu) iwapo adhabu itatoka baada ya michezo ya raundi ya 7 watakosa michezo ifuatayo Mudathir (Simba, Coastal, Mashujaa), Feisal (Mashujaa, Ihefu Mtibwa).


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA