BEKI LIVERPOOL ASHIKANA MASHATI NA KOCHA WAKE
Unaambiwa mlinzi wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho (33) ambaye kwasasa anakipiga Montpellier amegombana na kushikana mashati kocha wake Der Zakarian wakiwa mazoezini.
Ripoti inaeleza kuwa katika mazoezi yaliyofanyika jana (Jumanne) jioni Sakho alisusa na kuamua kutoka nje ya uwanja wa mazoezi mara baada ya kufanyiwa madhambi na kutopewa faulo, ambapo katika chumba cha kubadilishia nguo wawili hao walianza kubishana na ndipo Kocha huyo akamzomea kwa kumwambia "Cry-Baby" ndipo Sakho alipojibu kwa kumshika kola ya shati na kumwangusha chini kocha huyo mpaka pale wachezaji wengine walipoingilia kati.
Inaelezwa kuwa Sakho amekuwa kwenye wakati mgumu sana chini ya kocha huyo, ambapo msimu huu amecheza dakika 6 tu.