PHIRI ATUMA SALAMU KWA YANGA
Na Salum Fikiri Jr
Bao lililofungwa na mshambuliaji Moses Phiri dqkika ya 65 limeiwezesha Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ijefu SC ya Mbeya katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu bara.
Kwa matokeo hayo bado Simba inaendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya YƤnga lakini ikiwa na pointi 18 sawa na Yanga isipokuwa wanazidiwa magoli ya kufunga.
Simba ilianza kufunga bao la kwanza likiwekwa kimiani na Jean Baleke dakika ya 13 kabla ya Ihefu SC kusawazisha kupitia Ismail Mgunda dakika ya 25 kabla ya Phiri kufunga la ushindi.