MAPOKEZI YA MAKONDA YAFUNIKA
Mapokezi ya katibu mwenezi mpya wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Paul Makonda umezua balaa kwani idadi kubwa ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi.
Makonda alipokelewa ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo pia aliweza kuzungumza.
"Niseme tu kuanzia leo Oktoba 26, 2023, Taifa hili halina chama cha upinzani bali lina vyama vya watoa taarifa, na sisi kama chama tawala tutafanyia kazi taarifa zao kwa sababu ni chachu ya ujenzi si tu wa demokrasia bali wa maendeleo katika Taifa letu,"- Paul Makonda, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM