Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2023

MAYELE APIGA HAT TRICK UTURUKI

Picha
Mshambuliaji mpya wa timu ya Pyramids ya Misri amefunga mabao matatu peke yake hat trick katika mchezo wa kirafiki ambapo Pyramids i iliifunga mabao 7-0 Varsak ya Uturuki. Mabao mengine ya Pyramids yaliwekwa kimiani na Abdallah El Said, Mohamed Redaa na Ibrahim Adel

FEITOTO SIO PENDEKEZO LA KOCHA- KIEMBA

Picha
Na Salum Fikiri Jr “Mechi dhidi ya KMC ,Mkude na Lomalisa hawakuwa sehemu ya kikosi na walikaa jukwaani kabisa ,mechi ya juzi dhidi ya Asas Mkude alianza hapa utaona, Yanga ina wachezaji wengi wazuri na ina kocha mzuri kwa sababu kama Kocha sio mzuri ni ngumu kuwa manage hawa Wachezaji “ “Mimi nasema tu Yanga wana Kocha mzuri na atawapa kitu msimu huu” “Popat akiamka asubuhi anaenda wapi ? inawezekana akawa na ofisi sehemu nyingine je akienda anafanya kazi za Klabu au kazi zingine ?” “ Klabu inahitaji mtu ambaye ni full time sio akimaliza huku anarudi huku ? “ Shaffih Dauda Mchambuzi wa Clouds fm "Usajili wa Feisal ameupendekeza yeye (Dabo) ? Prisca ameuliza Kocha ni sehemu ya tatizo mimi nasema hapana tatizo ni mfumo angalia hata Wachezaji wakiingia Azam ule upambanaji unashuka anacheza lakini sio kiivyo ,mimi naona Azam shida ni mfumo na sio watu" “Hivi unajua kama mechi ya kwanza ya mashindano list ya wachezaji Kocha aliletewa akaibishia akaweka yake na ikafungwa “

AHMED ALLY AWEKA WAZI SIKU YA KUELEKEA ZAMBIA KUWAFUATA POWER DYNAMOS

Picha
Na Ikram Khamees Meneja wa Habari wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally amesema basi lao kuelekea Zambia kwa ajili ya kucheza na Power Dynamos litaondoka tarehe 13 Septemba saa 1 usiku na litafika Ndola, Zambia Septemba 15 na tarehe 17 Septemba baada ya mechi basi litaanza safari ya kurejea Tanzania. "Basi litaondoka nchini kwenda Zambia tarehe 13, Septemba saa 1 usiku na tutafika Ndola, Zambia tarehe 15, Septemba. Tarehe 17, Septemba baada ya mechi basi litaanza safari kurudi Tanzania. Kwa yeyote ambaye anataka kuungana nasi afike ofisini, kwa kila mtu gharama ni Tsh. 200,000 na anatakiwa kuwa na pasi ya kusafiria na kadi ya manjano. Mwisho wa kupokea nauli ni tarehe 10, Septemba."- amesema Ahmed Ally.

KMC YASHUSHA KIFAA KINGINE KUTOMA SOMALIA

Picha
Klabu Ya KMC Imekamilisha usajili wa kiungo wa Horseed Sc ya nchini Somalia. Abdulkarrim na chama lake la zamani la Horseed Sc walitolewa na APR ya Rwanda katika hatua ya awali ya CAFCL.. Ujio wake ni kutokana na ushawishi wa kocha wa KMC Moalin mwenye asili ya Somalia pia.. KMC wanapika kitu, mtu akiingia 18 zao atapokea kichapo cha kulipa mkono walioupokea kutoka kwa Wananchi Yanga SC

DJUMA SHABANI KUJIUNGA AZAM FC

Picha
Na Salmin Mrisho Baada ya klabu ya Yanga kuachana na nyota wake kutoka DRC Congo , Djuma Shaban mchezaji huyo yupo mbioni kujiunga na Azam Fc . Makubaliano binafsi tayari , nyota huyo anaweza kutambulishwa mda wowote kuanzia sasa .

SIMBA WAJIFUA VIKALI MO SIMBA ARENA

Picha
Kikosi cha wachezaji wa Simba SC kimeendelea kujifua katika uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju B jijini Dar es Salaam wakijiandaa na michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

GAMONDI ANATAKA KUFUNGA GOLI 10

Picha
Na Ikram Khamees Kocha mkuu wa klabu ya Young Africans Sports Club amefunguka na kusema kwamba bado yupo kwenye maandalizi na anategemea kufanya vizuri zaidi... . "Siyo lengo langu kufunga magoli matano kila mchezo, lakini wachezaji wangu wana njaa ya magoli .." "Mimi ninataka timu yangu ishambulie na kuzuia vizuri muda wote na ifunge magoli mengi huku ikicheza soka safi .. Bado tupo kwenye process mbeleni itacheza vizuri zaidi" - Miguel Gamondi, Kocha mkuu wa Yanga SC Kwamba 5G hajaridhika anataka yafike 10 au ?

MJUE IDDI NADO: KUTOKA MBEYA CITY HADI AZAM FC

Picha
Na Abdul Makambo Wakati anatoka Mbeya City Kujiunga na Azam fc alikua kwenye kiwango bora sana Alifanya Vyema alianza kuwatumia matajir hao wa Chamazi na Alikuwa mmoja wa Mawinga bora nchini Klabu nyingi zilimtamani na timu ya Taifa ikawa ni Uwanja wake wa Nyumbani kutokana na kiwango chake bora sana Ni moja ya Mawinga wa Kisasa ambao sifa zao sio Mbio tu bali Ubunifu,uwezo wa kuwatoka mabeki wakiwa wanalitafta lango Iddy Nado ni mmoja wa Mawinga Wachache ambao uwezo wao ni mkubwa sana. Kasi Ufundi Kufunga mabao Bahati Mbaya alikuja akapata Majeraha yakamuweka nje karbia msimu mmoja kama sio miwili Mwaka Jana akaanza taratibu kurejea kwenye kikosi lakin kama unavyojua majeraha ya Goti sio rahisi kurejea kwa kasi Akaanza kupewa muda lakin bado hakuonekana Nado kila mtu anayemjua lakin ndo kwanza alikua amerejea hivyo alihtaji mda kuwa sawa Kuisha kwa Ligi na Kwenda kujiandaa Kwa ajili ya msimu huu ni karata aliyoitumia vyema kurejea kwenye ubora wake... Msimu huu Tangu alipoanza kuamini...

JKT QUEENS WATWAA UBINGWA WA CECAFA

Picha
Klabu ya JKT Queens ya Tanzania imetwaa Ubingwa wa Kanda ya CECAFA kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa Wanawake. JKT imenyakua taji hilo baada ya kuifunga CBE Queens ya Ethiopia kwa mikwaju ya Penati 5-4 , dakika 120 walitoka 0-0 Hivyo JKT Queens itawakilisha ukanda wa CECEFA kwenye mashindano hayo ngazi ya fainali ambayo inatarajiwa kupigwa Nchini Ivory Coast kuanzia mwezi Novemba.

KIKOSI CHA STARS CHAITWA, CHAPAA TUJISIA

Picha
Na Prince Hoza Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kimeondoka leo kuelekea Tunis, Tunisia kwa Kambi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano kufuzu AFCON dhidi ya Algeria utakaochezwa Septemba 7, 2023 Algeria. . Wachezaji waliojumuhishwa kwenye kikosi hicho ni pamoja. 01. Beno Kakolanya — Singida 02. Metacha Mnata — Yanga 03. Erick Johora — Geita 04. Ibrahim Bacca — Yanga 05. Bakari Mwamnyeto — Yanga 06. Dickson Job — Yanga 07. Mzamiru Yassin — Simba 08. Sospeter Bajana — Azam 09. Clement Mzize — Yanga 10. Kibu Denis — Simba 11. Himid Mao — El Gaish 12. Mudathir Yahya — Yanga 13. Abdul Selemani Sopu — Azam 14. Abdulmalik Zakaria — Namungo 15. John Bocco — Simba 16. Kennedy Juma — Simba 17. Lameck Lawi — Coastal Union 18. Jonas Mkude — Yanga 19. Morice Abraham — Sobutica 20. Haji Mnoga — Aldershot 21. Ben Starkie — Basford 22. Simon Msuva — JS Kabylie 23. Novatus Dismas — Zulte Waregem 24. Mbwana Samatta — PAOK 25. Abdi Banda — Richards Bay

KOCHA POWER DYNAMOS AIGWAYA SIMBA

Picha
Baada ya kutinga Raundi ya Kwanza ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuing’oa African Stars ya Namibia kwa faida ya bao la ugenini na kutambua sasa itavaana na Simba SC, Kocha Mkuu wa Power Dynamos ya Zambia, Mwenya Chipepo ameonekana kuingiwa ubaridi akisema anawafahamu vizuri wapinzani wao ili na sasa wanajipanga upya kuvunja rekodi ya Wekundu hao. Dynamos imetinga hatua hiyo baada ya awali kufungwa 2-1 ugenini kisha jumamozi (Agosti 26) ikalipa kisasi nyumbani kwa kushinda 1-0 na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 2-2 na kupenya kwa kanuni ya faida ya bao la ugenini na itavaana na Simba SC mwezi ujao ikiwa ni mwezi mmoja tangu zikutane kwenye pambano la kirafiki la kimataifa kwenye Tamasha la Simba Day na miamba hiyo ya Zambia kulala 2-0 Kwa Mkapa. Akizungumza kutoka nchini Zambia, Chipepo alisema sio wageni kwa Simba SC, wanaifahamu vizuri kuanzia ubora wao wa timu na rekodi zao kwenye michuano hiyo, hivyo wanajipanga ili kuivunja, kwani kwa miaka ya hivi karibuni, Simba SC imekuw...

KRAMO AOMBA KUONDOKA SIMBA, KISA YAO, PACOME

Picha
Na Abdul Makambo Taarifa zikufikie inasemekana kiungo mshambuliaji Aubin Kramo raia wa Ivory Coast ameuomba uongozi wa klabu ya Simba wamruhusu aondoke klabu hiyo arudi kwao au wamtoe kwa mkopo kwa sababu kuna mambo hayaelewi kwenye timu hiyo. Kramo anadai ka inapofika siku ya mechi anajikuta anaumwa alafu mechi ikiisha anakuwa sawa. Mchezaji huyo jana ameanza mazoezi na wenzake lakini hana raha tangu alipojiunga na Wekundu hao wakati anawaona marafiki zake Kouassi Yao Attohoula na Zouzoua Pacome waliopo Yanga wanafurahia maisha

WANGEBAKI WCB WANGEKUWA MBALI ZAIDI- MKUBWA FELLA

Picha
Mkubwa Fella amesema Baada ya Harmonize na Rayvanny kutoka WCB wanajitahidi kwa kiasi chake japokuwa siyo kama walivyowatabiria wao, amesema kama wangebakia WCB wangekuwa mbali zaidi ingawa bado hawako nyuma. Mkubwa ambaye ni Meneja wa WCB ameongeza kuwa Rayvanny anajitahidi zaidi kuliko Harmonize. Mkubwa Fella Harmonize Rayvanny

FIFA YAIFUNGIA YANGA, KISA BIGIRIMANA

Picha
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo. Birigimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee) ambapo klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo. Wakati FIFA imeifungia Yanga kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani. TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili. “Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.” TFF

JKU YAMUONDOA PLUIJM SINGIDA FG

Picha
Klabu ya Singida Fountain Gate Fc, imethibitisha kuachana na Kocha wao Hans van der Pluijm kwa makubaliano ya pande zote mbili Kupitia taarifa yake kwa umma Singida Fontaine Gate imebainisha kuwa hivi sasa Timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi Mathias Lule mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.

WENYE LIGI YAO WAREJEA KILELENI NA MWENDO WA 5, 5

Picha
Na Asher Maliyaga Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara usiku wa leo imerejea kileleni baada ya kuikandamiza mabao 5-0 timu ya JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo Yanga inaishusha kileleni Azam FC ambayo jana iliishusha kileleni Simba, hata hivyo Yanga inakuwa juu kwa uwiano wa mabao ya kufunga kwani mpaka sasa ina mabao 10 na pointi 6, wakati Azam na Simba nazo zina pointi 6. Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na Stepano Aziz Ki dakika ya 45, Kennedy Musonda dakika ya 54, Yao Kouasi dakika ya 64 na Maxi Nzengeli aliyefunga mawili dakika za 79 na 87. Yanga inayonolewa na Muargentina Manuel Angel Gamondi bado inaendelea kusifika kwa kucheza kandanda safi .

SIMBA YAACHANA NA BANDA

Picha
Mchezaji Peter Banda baada ya kuachana klabu ya Simba Sc, njiani kuhamia FC Kyrvbas. Mpaka wakati huu mazungumzo yamekamilika kuhusu uhamisho wake Peter Banda. Anachosubiria ni visa yake ya kusafiri kwenda Ukraine, inaelezwa itakuchukua hadi mwezi mmoja.

FC BAYERN YAINGIA MKATABA NA VISIT RWANDA

Picha
Baada ya PSG, Arsenal, Rwanda sasa imeingia makubaliano na klabu ya Bayern Munich kupitia kampeni yao ya Visit Rwanda kwa mkataba wa miaka mitano. Ushirikiano huo utajumuisha kuanzisha Academy nchini Rwanda na timu kutoka Rwanda itapata Nafasi ya kushiriki Michuano ya Vijana ya FC Bayern. V isit Rwanda itaonekana kwenye uwanja, jezi na tovuti za Bayern Munich

AZAM FC YAISHUSHA SIMBA KILELENI

Picha
Na Salum Fikiri Jr Azam FC imeishusha Simba kwenye nafasi ya kwanza baada ya usiku huu kuishushia kipigo kitakatifu maafande wa Tanzania Prisons ya Mbeya mabao 3-1 mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 6 ikiwa imecheza mechi mbili, mabao ya Azam yalifungwa na Prince Dube dakika ya 11 kipindi cha kwanza, Iddi Nado dakika ya 47 na Nathanael Chilambo dakika ya 83 kipindi cha pili. Goli la kufutia machozi la Prisons limefungwa na Zabona Mayombya dakika ya 90, ligi hiyo inaendelea kesho ambapo mabingwa watetezi ya ligi hiyo Yanga SC wataikaribisha JKT Tanzania .

HONGERA RAIS MWINYI KWA KURUDISHA MASUMBWI ZANZIBAR

Picha
Na Prince Hoza HII mara yangu ya pili kumpongeza Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hussein Ally Mwinyi kwa kurudisha mchezo wa masumbwi, lakini leo nipo tofauti na mara ya kwanza nilipoandika pongezi kwa kurudisha mchezo huo.  Pongezi za mara ya pili ni kwa mchezo huo kuchezwa rasmi visiwani humo, wakati Serikali ya Mapinduzi ikitangaza kuurudisha mchezo huo, imechukua mwaka sasa hakuna pambano lolote lililowahi kufanyika.  Agosti 27 kuliandaliwa pambano la masumbwi lililowakutanisha mabondia kutoka Zanzibar na Tanzania bara, kufanyika kwa pambano hilo ambapo ni baada ya miaka 60 bila radhaa ya mchezo wa masumbwi hatimae historia ya ngumi kutoka visiwani Zanzibar imerejea.  Kampuni ya Tosh Sports Promotion kwa kushirikiana na Kamisheni ya ngumi visiwani Zanzibar pamoja na Azam Media Limited imeuleta mchezo wa ngumi Zanzibar kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi.  Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla imeshuhudia usiku wa kipekee wa ngumi kwa pambano kuu la bondia Ibrahim Class...

TIMU YA BARAKA MAJOGOLO YAPATA USHINDI AFRIKA KUSINI

Picha
Kiungo wa kimataifa Rastaman Baraka Gamba Majogoro Jana amecheza mchezo wake wa kwanza CHIPPA United dhidi ya na timu ya ,imepata ushindi wake wa kwanza katika ligi kuu ya Afrika kusini kwa mara ya kwanza. Klabu yake imecheza mechi Tano wamepata sare tatu dhidi ya Orlando Pirates,TS Galaxy pamoja na Kaizer Chiefs Jana yeye ndiyo mchezo wake wa kwanza na amecheza kwa dakika zote 90 timu yake Chippa United imepata ushindi wa kwanza kwa kumfunga Cape Town Spurs kwa goli moja kwa sifuri.

JULIO AWAPIGIA CHAPUO MATOLA, MGUNDA

Picha
Na Mwandishi Wetu "Mimi siogopi kusema ukweli maana naona Azam ina kila kitu, lakini haifanyi vizuri kwa kuwa watu wanaopewa majukumu kuivusha hawawezi, wawape timu watu sahihi ambao wanaujua utendaji lakini wao wanapeana kazi kishkaji sana na ndicho kinachowafelisha" "Kwa miundombinu iliyonayo Azam hata ikinolewa naye, Juma Mgunda au Seleman Matola wanaweza kuifikisha mbali ikiwemo kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara nyingine kwani ina kila kinachohitajika" "Wachezaji wanaosajiliwa ni kama hawajitambui na wamekuwa wakiridhikia na pesa nyingi wanazolipwa kwa vile hawana presha wanayopewa kuwafanya wapambane" "Kwa wanavyocheza uwanjani ukiitazama na Yanga iliyoweka kambi Avic Town Dar es Salaam na Azam iliyotumia pesa nyingi kwenda Tunisia utaona vitu viwili tofauti" "Yaani Yanga utasema wao ndio walikuwa nje ya nchi kutokana na ubora wa soka wanalocheza kumbe hapana, ila hawa waliosafiri kambi ya wiki mbili, lakini wanapoteza muda mwingi njiani...

JKU YALIPA KISASI, LAKINI SINGIDA WAMEFUZU RAUNDI YA KWANZA

Picha
Na Ikram Khamees Licha ya kupata ushindi wa mabao 2-0 JKU imeondolewa katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hasa baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 4-3 na timu ya Singida Fountain Gate. Bahati haikuwa yao vijana wa JKU ambao kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kufanikiwa kuongoza mabao 2-0 lakini kipindi cha pili Singida Fountain Gate walibadilika na kuzuia wasifungwe bao la tatu ambalo lingewaondoa mashindanoni.

BEKI WA YANGA KIMEELEWEKA DR CONGO

Picha
Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ametua DR Congo  na jana alitarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Lubumbashi Sport, akiungana na George Mpole anayecheza nchini humo kwenye klabu ya FC Lupopo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka DR Congo, beki huyo tayari alishatua nchini humo tangu Jumatano na juzi alitembezwa kuonyeshwa mandhari ya klabu hiyo kabla ya jana kutakiwa kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo iliyopo katika Ligi Kuu ya Dr Congo maarufu Linafoot.

YANGA KUANZIA UGENINI LIGI YA MABINGWA

Picha
Na Ikram Khamees Taarifa njema kwa Mashabiki wa Yanga ni kuwa mchezo wao unaofuata wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh wataanzia ugenini kisha kumalizia nyumbani. Klabu ya Al Merreikh wanatumia mechi zao za nyumbani katika nchi ya Rwanda  hivyo Yanga wataenda Rwanda kisha kumalizia Tanzania.

TIMU YA ZAMANI YA ROBERTINHO YAONDOSHWA LIGI YA MABINGWA

Picha
Klabu ya Vipers jana wameaga Michuano ya CAF CL baada ya Kutolewa na Jwaneng Galaxy Mchezo wa jana Vipers wameshinda 2️ kwa 1️ ushindi ambao haukuwa na faida kwao kwa maana mechi ya kwanza kule Botswana walipoteza[2-0] Hivyo Jwaneng Kupata Bao St Mary's ni Faida iliyowapeleka moja kwa moja hatua inayofuata na Watakutana na O.Pirates kutoka Afrika Kusini... Haijawa siku nzuri kwa Vipers kwa maana walionekana kama wanaumaliza mchezo mara baada ya kwenda mapumziko wakiongoza[2-0]

FAR RABAT YA NABI YAFUZU LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Picha
Na Mwandishi Wetu Mabingwa wa Morocco Far Rabat Wanaonelewa na kocha wa Zamani wa Yanga sc Nasreddine Nabi wamefuzu hatua ya pili ya CAFCL Hatua iyo inafuata baada ya kuwaondosha A.Kara ya nchini Togo kwa Matokeo ya Jumla Bao 8-0. Mchezo wa Kwanza Ugenini Far Rabat walishinda [1-0] kabla ya kumshushia mtu week leo hii nchini Morocco [7-0] Ushindi Huo unawahakikishia Far Rabat nafasi ya kusonga mbele hatua inayofuata kabla ya kufuzu hatua ya makundi Far Rabat watakutana na Mabingwa Wa Tunisia Etoile du sahel Kibarua kingne kwa Prof Nabi.. FAR RABAT VS ETOILE DU SAHEL Mshindi wa matokeo ya Jumla Atajihakikishia Ticket ya kufuzu makundi moja kwa moja Mechi za Waarabu kwa Waarabu tena ktk mechi ya Maamuzi huwa raha sana figisu wanafanyiana na vurugu juu acha tuone. Etoile Du Sahel ni wamoto sana msimu huu na walipania sana kurejea katika ramani ya soka, ni atasonga mbele ni jambo la kusubiri na kuona

BUSU LAMPONZA RAIS WA SOKA HISPANIA

Picha
Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) limemsimamisha kwa muda wa siku 90 Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Uhispania ndugu Luis Rubiales kufuatia kipande cha video kilichomuonesha akimpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania Jennifer Hermoso wakati wakisherehekea Ubingwa wa Kombe la dunia la wanawake. Bwana Luis Rubiales amesimamishwa kutojihusisha na shughuli zozote zinazohusu mpira kwa ngazi ya Kitaifa na kimataifa kwa mda huo ambapo kamati ya nidhamu ya FIFA itakaa kumfanyia uchunguzi zaidi.