MJUE IDDI NADO: KUTOKA MBEYA CITY HADI AZAM FC
Na Abdul Makambo
Wakati anatoka Mbeya City Kujiunga na Azam fc alikua kwenye kiwango bora sana
Alifanya Vyema alianza kuwatumia matajir hao wa Chamazi na Alikuwa mmoja wa Mawinga bora nchini
Klabu nyingi zilimtamani na timu ya Taifa ikawa ni Uwanja wake wa Nyumbani kutokana na kiwango chake bora sana
Ni moja ya Mawinga wa Kisasa ambao sifa zao sio Mbio tu bali Ubunifu,uwezo wa kuwatoka mabeki wakiwa wanalitafta lango
Iddy Nado ni mmoja wa Mawinga Wachache ambao uwezo wao ni mkubwa sana.
Kasi
Ufundi
Kufunga mabao
Bahati Mbaya alikuja akapata Majeraha yakamuweka nje karbia msimu mmoja kama sio miwili
Mwaka Jana akaanza taratibu kurejea kwenye kikosi lakin kama unavyojua majeraha ya Goti sio rahisi kurejea kwa kasi
Akaanza kupewa muda lakin bado hakuonekana Nado kila mtu anayemjua lakin ndo kwanza alikua amerejea hivyo alihtaji mda kuwa sawa
Kuisha kwa Ligi na Kwenda kujiandaa Kwa ajili ya msimu huu ni karata aliyoitumia vyema kurejea kwenye ubora wake...
Msimu huu Tangu alipoanza kuaminiwa Tumeanza kumuaona Iddy Nado wa Wa Mbeya City,Nado wa Azam fc msimu wa kwanza akiwa ametoka Mbeya City....
Ni Dhahiri Gari la Iddy Limewaka sana na Binafsi mie ni shabiki wake sana tangu akiwa Mbeya Ule mwendo wake na uwezo wa Kuwatoka Mabeki ndo Vitu Nilivutiwa navyo 👏👏👏
This Time round Karudi vyema Na Mungu Amsaidie Aepukane na Majeraha Ili Tufurahia kipaji chake bora sana..
Taratibu ameanza kujikatia kipande chake ndani ya kikosi cha kwanza cha Azam fc na akiendelea hivi hakuna wa kumuweka Nje..👇
Anatengeneza magoli kwa wenzie
Anafunga pale inapobidi
Sio Kipenzi cha Mabeki wasio na kasi
Ukitaka Mwendo na Ufundi atakupa tena zaidi na zaidi.