HONGERA RAIS MWINYI KWA KURUDISHA MASUMBWI ZANZIBAR
Na Prince Hoza
HII mara yangu ya pili kumpongeza Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hussein Ally Mwinyi kwa kurudisha mchezo wa masumbwi, lakini leo nipo tofauti na mara ya kwanza nilipoandika pongezi kwa kurudisha mchezo huo.
Pongezi za mara ya pili ni kwa mchezo huo kuchezwa rasmi visiwani humo, wakati Serikali ya Mapinduzi ikitangaza kuurudisha mchezo huo, imechukua mwaka sasa hakuna pambano lolote lililowahi kufanyika.
Agosti 27 kuliandaliwa pambano la masumbwi lililowakutanisha mabondia kutoka Zanzibar na Tanzania bara, kufanyika kwa pambano hilo ambapo ni baada ya miaka 60 bila radhaa ya mchezo wa masumbwi hatimae historia ya ngumi kutoka visiwani Zanzibar imerejea.
Kampuni ya Tosh Sports Promotion kwa kushirikiana na Kamisheni ya ngumi visiwani Zanzibar pamoja na Azam Media Limited imeuleta mchezo wa ngumi Zanzibar kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi.
Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla imeshuhudia usiku wa kipekee wa ngumi kwa pambano kuu la bondia Ibrahim Class Mgender a k a King Class Mawe dhidi ya Hamis Muathai walioandika historia ya kwanza ya ufunguzi wa mchezo wa masumbwi visiwani Zanzibar.
Mabondia Class na Hamisi watacheza pambano la raundi 8 kwenye uzito wa lightwigh kg 61 lisilo la ubingwag.
Class anarudi kwenye pambano hili tangu alivyocheza pambano lake la mwisho hapa jijini Dar es Salaam tarehe 25/5/2023 dhidi ya mpinzani wake Said Chino a k a Bull Dog.
Pambano la ubingwa wa taifa kwenye uzito wa Super Featherweight kg 58 na alifanikiwa kushinda pambano hilo kwa majaji wote watatu.
Pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yaliyo sherehesha rasmi kurejea kwa ngumi katika visiwa vya Zanzibar mabondia kama Karim Mandonga na Dullah Mbabe walikuwepo kwenye mapambano hayo yatakayofanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Sung visiwani Ungujo ndipo yalipigwa mapambano yote.
Class alienda kwenye pambano hilo akiwa na rekodi ya jumla ya mapambano 36 kashinda 30 kwa ko 14 kapoteza 6 na sare 0, historia iliandikwa Agosti 27.
Bila shaka natumia nafasi hii tena kumpa hongera Rais huyu wa Zanzibar kwani wamepita Marais sita kushindwa kuurejesha mchezo huo.
Rais wa awamu ya kwanza wa Zanzibar Abeid Amaan Karume ndie aliyeupiga marufuku mchezo huo mwaka 1963 hasa baada ya Uhuru kutoka kwa Uingereza na Sultan wa Oan aliyeitawala kwa rane kadhaa zilizopita.
Rais Karume aliuzuia mchezo huo akidai hauna maana yoyote na ni mchezo wa kitumwa kwani wakoloni waliwashindanisha watumwa ili kupata mlo au kitu chochote hivyo watumwa pekee waliingia ulingoni huku mkoloni akikaa kwenye kiti kuangalia mpambano.
Hivyo Karume alipofanikiwa kuikomboa Zanzibar akasitisha mchezo huo, Rais Mwinyi amekuwa Rais wa kwanza kuurudisha mchezo huo baada ya Uhuru.
ALAMSIKI