AZAM FC YAISHUSHA SIMBA KILELENI
Na Salum Fikiri Jr
Azam FC imeishusha Simba kwenye nafasi ya kwanza baada ya usiku huu kuishushia kipigo kitakatifu maafande wa Tanzania Prisons ya Mbeya mabao 3-1 mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 6 ikiwa imecheza mechi mbili, mabao ya Azam yalifungwa na Prince Dube dakika ya 11 kipindi cha kwanza, Iddi Nado dakika ya 47 na Nathanael Chilambo dakika ya 83 kipindi cha pili.
Goli la kufutia machozi la Prisons limefungwa na Zabona Mayombya dakika ya 90, ligi hiyo inaendelea kesho ambapo mabingwa watetezi ya ligi hiyo Yanga SC wataikaribisha JKT Tanzania
.