BUSU LAMPONZA RAIS WA SOKA HISPANIA
Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) limemsimamisha kwa muda wa siku 90 Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Uhispania ndugu Luis Rubiales kufuatia kipande cha video kilichomuonesha akimpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania Jennifer Hermoso wakati wakisherehekea Ubingwa wa Kombe la dunia la wanawake.
Bwana Luis Rubiales amesimamishwa kutojihusisha na shughuli zozote zinazohusu mpira kwa ngazi ya Kitaifa na kimataifa kwa mda huo ambapo kamati ya nidhamu ya FIFA itakaa kumfanyia uchunguzi zaidi.