AHMED ALLY AWEKA WAZI SIKU YA KUELEKEA ZAMBIA KUWAFUATA POWER DYNAMOS
Na Ikram Khamees
Meneja wa Habari wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally amesema basi lao kuelekea Zambia kwa ajili ya kucheza na Power Dynamos litaondoka tarehe 13 Septemba saa 1 usiku na litafika Ndola, Zambia Septemba 15 na tarehe 17 Septemba baada ya mechi basi litaanza safari ya kurejea Tanzania.
"Basi litaondoka nchini kwenda Zambia tarehe 13, Septemba saa 1 usiku na tutafika Ndola, Zambia tarehe 15, Septemba. Tarehe 17, Septemba baada ya mechi basi litaanza safari kurudi Tanzania.
Kwa yeyote ambaye anataka kuungana nasi afike ofisini, kwa kila mtu gharama ni Tsh. 200,000 na anatakiwa kuwa na pasi ya kusafiria na kadi ya manjano.
Mwisho wa kupokea nauli ni tarehe 10, Septemba."- amesema Ahmed Ally.