FC BAYERN YAINGIA MKATABA NA VISIT RWANDA
Baada ya PSG, Arsenal, Rwanda sasa imeingia makubaliano na klabu ya Bayern Munich kupitia kampeni yao ya Visit Rwanda kwa mkataba wa miaka mitano.
Ushirikiano huo utajumuisha kuanzisha Academy nchini Rwanda na timu kutoka Rwanda itapata Nafasi ya kushiriki Michuano ya Vijana ya FC Bayern.
Visit Rwanda itaonekana kwenye uwanja, jezi na tovuti za Bayern Munich