FIFA YAIFUNGIA YANGA, KISA BIGIRIMANA
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
Birigimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee) ambapo klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.
Wakati FIFA imeifungia Yanga kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.
TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.
“Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.” TFF