JKT QUEENS WATWAA UBINGWA WA CECAFA
Klabu ya JKT Queens ya Tanzania imetwaa Ubingwa wa Kanda ya CECAFA kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa Wanawake.
JKT imenyakua taji hilo baada ya kuifunga CBE Queens ya Ethiopia kwa mikwaju ya Penati 5-4 , dakika 120 walitoka 0-0
Hivyo JKT Queens itawakilisha ukanda wa CECEFA kwenye mashindano hayo ngazi ya fainali ambayo inatarajiwa kupigwa Nchini Ivory Coast kuanzia mwezi Novemba.