Kwa habari na matangazo tunapatikana Kariakoo jijini Dar es Salaam au piga +255 652 626627 au +255 755 522 216 barua pepe princehoza@gmail.com
SIMBA WAJIFUA VIKALI MO SIMBA ARENA
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
-
Kikosi cha wachezaji wa Simba SC kimeendelea kujifua katika uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju B jijini Dar es Salaam wakijiandaa na michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe
Na E xipedito Mataruma, MBEYA SIMBA SC imeshindwa kupata saini ya mshambuliaji wa Prisons ya Mbeya Jeremia Juma Mgunda mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga Juma Mgunda. Jeremia Juma mmoja kati ya washambuliaji hatari waliobuka msimu uliopita, alifanikiwa kupachika mabao 14 akiwa nyuma ya Mzimbabwe Donald Ngoma wa Yanga. Mchezaji huyo ambaye amepanda kwa kasi msimu uliopita yupo tayari kutua Simba lakini kikwazo ni dau dogo linalotaka kutolewa na klabu hiyo ya Simba. Akizungumza na mtandao huo mshambuliaji huyo wa timu ya Prisons amesema yupo tayari kuichezea Simba msimu ujao lakini sio kwa kiasi kidogo cha pesa ambacho wanataka kumpa. Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 14 msimu uliopita na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ameiambia Mambo Uwanjani kama Simba wamepanga kumpa shilingi Mil 20 hayupo tayari na ni vyema akabakia Prisons ili aendelee kubaki kwenye ajira yake ya uaskari Magereza. "Bado naendelea kuzungumza na vio...
Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...