BEKI WA YANGA KIMEELEWEKA DR CONGO
Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ametua DR Congo na jana alitarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Lubumbashi Sport, akiungana na George Mpole anayecheza nchini humo kwenye klabu ya FC Lupopo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka DR Congo, beki huyo tayari alishatua nchini humo tangu Jumatano na juzi alitembezwa kuonyeshwa mandhari ya klabu hiyo kabla ya jana kutakiwa kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo iliyopo katika Ligi Kuu ya Dr Congo maarufu Linafoot.